JKT Queens yaua 16-0, Simba Queens yabanwa

Muktasari:

Pia nao Evergreen waliingia uwanjani wakikumbuka vipogo viwili mfululizo walivyopata mbele ya Simba Queens kwa mabao 6-0 kisha kudundwa 9-0 na JKT Queens.

Mwanza. Kwa mara nyingine tena kikosi cha Marsh Queen kimeshindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Evergreen katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake huku JKT Queens ikiishushia kipigipo Mapinduzi Queens mabao 16-0.
Mchezo huo ambao umepigwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini hapa ukiwa wa tatu katika Ligi hiyo,ilishuhudiwa wenyeji wakilazimishana sare hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga Princess kwa kichapo cha bao 1-0.
Pia nao Evergreen waliingia uwanjani wakikumbuka vipogo viwili mfululizo walivyopata mbele ya Simba Queens kwa mabao 6-0 kisha kudundwa 9-0 na JKT Queens.
Katika mechi ya leo Marsh ndio walitangulia kuandika bao katika dakika ya pili lililofungwa na Abinus Omary,bao ambalo lilisawazishwa na Irine Mtow dakika ya 36.
Kwa matokeo hayo Marsh wanafikisha pointi nne huku Evergreen wakifikisha alama moja baada ya timu zote kucheza mechi tatu.

MATOKEO YOTE HAYA HAPA

LIKI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI LITE

Simba Quees 1-1 Alliance

Panama FC 5-0 Baobab Queens

JKT Quees 16-0 Mapinduzi Queens

Marsh Queens- Evergreen Queens

Mlandizi Queens 0-0 Sisterz FC