JKT Queens wababe kila kona

Muktasari:

Twiga Stars inatarajia kuingia kambini kesho Alhamisi kujiandaa kufuzu Olympic ambapo watacheza na DR Congo, Aprili 5 hapa Tanzania ugenini itakuwa Aprili 9.

KOCHA wa JKT Queens, Ali Ali amesema kitendo cha wachezaji wake 12 kuitwa kwenye kikosi cha Twiga Stars, kinamfanya ajijue thamani yake kazi yake kwamba imetambulika na taifa.
Wachezaji kutoka JKT Queens ambao wameitwa kwenye kikosi cha Twiga Stars ni Fatuma Omar Jawadu, Najiath Idrissa, Maimuna Hamis, Fatuma Salum,Happiness Hezron, Stumai Abdallah, Annastazia Antony, Fatuma Makusanya, Donisia Minja, Fatuma Mustapha, Asha Rashid na Zena Khamis.
"Sio jambo dogo wachezaji kuitwa 12 kwenye kikosi cha Twiga Stars, nimefariji na pia imeniongezea kujituma zaidi kufanya kazi yangu iwe na thamani kubwa.
"Haina maana kwamba timu ambazo zimetoa wachezaji wachache ama hazijatoa kabisa sio nzuri kwenye ligi yetu hapana zina ushindani wa hali ya juu na bila shaka awamu nyingine wataitwa wao,"anasema.
Twiga Stars inatarajia kuingia kambini kesho Alhamisi kujiandaa kufuzu Olympic ambapo watacheza na DR Congo, Aprili 5 hapa Tanzania ugenini itakuwa Aprili 9.