VIDEO: JB ana kazi maalumu Simba na AS Vita

Muktasari:

JB ambaye aliingia Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni huku mechi ya Simba na AS Vita ikitarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movie, Jacob Steven 'JB' amesema katika mchezo wa leo Jumamosi kati ya Simba na AS Vita ana kazi maalumu na ndiyo maana amefika uwanjani mapema.

JB ambaye aliingia Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni huku mechi ya Simba na AS Vita ikitarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.

Aliingia na kwenda moja moja kwenye jukwaa la VIP B upande ambao huwa wanakaa mashabiki wa Simba akaungana na jamaa wengine.

"Kuwahi kwangu uwanjani kuna sababu, leo nina kazi maalumu ya kufanya hapa,"alisema JB ambaye anajulikana pia kwa jina la utani la Bonge Bwana. Akiizungumzia Simba msanii huyo ambaye alikuwa amevalia jezi nyekundu ya klabu hiyo alisema.

"Ushindi leo ni lazima kwa Simba subiri mtaona,"alisema JB.