Ismailia yamchomoa mshambuliaji Azam

Muktasari:

Zayd amekuwa akifuatiliwa na Ismailia kwa muda mrefu na sasa wanaonekana kukaribia kukamilisha usajili wake.

Mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Zayd yuko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wake na klabu ya Ismailia ya Misri.
Makamu Mwenyekiti wa Azam FC Abdulkarim Amin 'Popat' amesema dili hilo lipo katika hatua za mwisho kukamilishwa.
Popat amesema kwasasa klabu yao ipo katika mazungumzo ya mwisho na Ismailia katika kumsajili Zayd.
Amesema Zayd bado alikuwa na mkataba wa miaka mitatu na klabu yao na kwamba wakati wowote kutoka sasa atasafiri kuelekea Misri.
Endapo dili hilo litakamilika Zayd ataungana na nahodha wake na kiungo wa Azam nchini humo Himid Mao ambaye anaichezea Petrojet ya nchini humo.