Ishu ya Kakolanya yatikisa

Tuesday February 19 2019

 

By Thomas Ng'itu

SAKATA la Beno Kakolanya na klabu yake ya Yanga, limezidi kushika kasi baada ya mwanasheria wa mchezaji huyo, Leonard Richard kufikisha suala la mteja wake Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Kakolanya amekuwa kwenye mvutano tangu mwaka jana, baada ya kipa huyo kujiondoa kikosini akishinikiza kudai malimbikizo ya mishahara yake pamoja na pesa ya usajili.

Mwanasheria huyo aliliambia Mwanaspoti kwamba, walikuwa wakipelekeana barua na uongozi wa Yanga ili kutatua suala hilo kama ambavyo walikubaliana, lakini baadaye mambo yamekuwa tofauti.

“Tulikuwa tunakubaliana kwa maandishi, lakini uongozi umekuwa ukiniyumbisha kufanya maamuzi.”

Aliongeza kwamba hata barua yao ya mwisho ambayo walipelekewa Yanga, walishindwa kutoa majibu kwa muda waliokubaliana.

Advertisement