Huyu ndo Mcape Verde aliyeifunga Taifa Stars

Muktasari:

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Taifa Stars ilifungwa mabao mawili ya haraka na mshambuliaji mmoja anayeitwa Ricardo Gomes na hii ndiyo historia yake.

Dar es Salaam. Timu ya Taifa Stars imepigwa mabao mawili ya haraka katika dakika 45, za mwanzo za mchezo huo na straika, Ricardo Gomes wa Cape Verde.

Historia ya mchezaji huyo amezaliwa Desemba 18, 1991 na sasa ana miaka 26. Alizaliwa katika mji wa Praia nchini Cape Verde.

Ana urefu wa futi 6 na nchi 2. Nafasi anayomudu kucheza ni mshambuliaji wa kati.

Kwa sasa anacheza soka nchini Serbia katika Klabu ya Partizan. Jezi anayovaa katika klabu yake ni namba 11, na kwenye timu yake ya taifa ni 17.

TIMU ZA VIJANA

Aliichezea Vizela ya nchini humo kuanzi mwaka 2009–2010, baada ya hapo alipandishwa timu ya wakubwa.

TIMU KUBWA

Aliichezea Klabu ya Vizela iliyompandisha msimu wa 2010 na 2013 aliondoka na kutimkia nchini Ureno alikojiunga na Klabu ya Vitória Guimarães kwa mwaka 2013, aliyoicheza mpaka 2016.

Aliachana nao baada ya Nacional kupanda dau na kumchukua kwa mkopo ambapo mwaka huo huo waliamua kumnunua jumla.

Akiwa na timu hiyo ya Nacional alicheza kwa miaka miwili msimu wa 2016, mpaka 2018 ndipo akahamisha makazi na kwenda Serbia katika klabu hiyo ya Rartizan anayoichezea mpaka sasa.