Huyu ndiye Igangula wa Yanga

Muktasari:

Mbali na nafasi hizo za uongozi ambazo amewahi kuongoza nyingine ni Rais wa wabunifu wamajengo Afrika mashariki (EAIA), kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.

MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti Yanga, Mbaraka Hussein Igangula ameweka wazi namna ambavyo amekuwa na uzoefu wa kutosha katika kuongoza.
Igangula amesema amewahi kuwa Mwenyekiti wa TAMICO Kanda ya Pwani (Dar es Salaam,  Pwani, Morogoro,Lindi na Mtwara)  kuanzia mwaka 2002 hadi 2006.
"Nimewahi pia kuwa Rais wa wabunifu majengo Tanzania (AAT),  kuanzia mwaka 2012 hadi 2018," alisema Igangula.
Mbali na nafasi hizo za uongozi ambazo amewahi kuongoza nyingine ni Rais wa wabunifu wa majengo Afrika mashariki (EAIA), kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.
Makamu Rais wa Chama cha Meneja Miradi (PMAT), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (TUCTA), Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Migodi na Ujenzi, Nishati (TAMICO) na kazi nyinginezo.
Mjumbe wa bodi ya serikali ya kima cha chini cha mishahara sekta binafsi mpaka sasa, mjumbe wa bodi ya chuo kikuu ardhi, kitengo cha ubunifu majengo (SADE) kuanzia mwaka 2011 hadi 2013.
Pamoja na mjumbe wa bunge maalum la katiba mwaka 2014.

ELIMU YAKE
Igangula anashahada ya uzamili, cheti cha kimataifa (In Architecture, Energy and environment), Diploma ya juu ya ubunifu majengo, diploma ya usanifu majengo,elimu ya kidato cha sita, cheti cha kidato cha nne, cheti cha meneja miradi na cheti cha usuluhishi.