Huyu Mkoma yuko vizuri aisee!

Muktasari:

  • Hamisi Ramadhani Mkoma anayegombea nafasi ya ujumbe kwenye uchaguzi mkuu wa Simba unaotarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu, hatakuwa cha kuhofia kwenye kampeni zao za kujinadi kwani ana vigezo vyote na pia amewahi 2010 amewahi kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji na mwaka 2011 pia aligombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

WAKATI uchaguzi mkuu wa Simba ambao lengo ni kuwapata wajumbe saba watakaingia moja kwa moja kuiwakilisha klabu upande wa wanachama kwenye Bodi ya Wakurugenzi, ukipamba moto mambo yamezidi kunoga.

Uchaguzi huo unafanyika Novemba 4, mwaka huu ambapo kampeni za wagombea zimepangwa kuanza Oktoba 26.

Wanachama wa Simba wanapaswa kuchagua viongozi saba, mmoja Mwenyekiti na wajumbe sita. Mwanaspoti linakuletea mwendelezo wa sifa za wagombea hao ili kuwawezesha wanachama kupata mwanga wa kiongozi gani wa kwenda naye kwa kuzingatia elimu, uzoefu na mikakati yao kabla ya kuanza kujinadi kuomba kura.

Hamisi Ramadhani Mkoma

Mkoma (51) ni mwanachama wa Simba mwenye kadi namba 01434 anaishi jijini Dar es Salaam.

Mkoma alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Turian (1976-7982), alijiunga na elimu ya sekondari shule ya Kinondoni kuanzia mwaka 1983-1986.

ELIMU YA JUU

Mwaka 1987-1989 alijiunga na Chuo cha CDTI-Tengeru ambako alipata Astashahada ya Maendeleo ya Jamii, baadaye mwaka 1992-1995 alijiendeleza chuoni hapa akichukuwa Stashahada ya juu ya Maendeleo ya Jamii.

Mwaka 1997-1998 alipata Stashahada ya Uzamili ya Mipango ya Mikoa (IRDP- Dodoma) na baadaye alichukuwa

Shahada ya Uzamili ya Biashara za kimataifa (Masters degree in International Business) katika chuo cha Indian Institute of Foreign Trade (IIFT) mwaka 2004-2006.

Uzoefu katika soka

Mkoma aliwahi kuwa nahodha wa timu ya Chuo CDTI - Tengeru kwa kipindi chote alikuwa anasoma chuoni hapo, ni

Mwenyekiti Mabibo United FC kuanzia mwaka 2000 mpaka sasa.

Mwaka 2007-2010 alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu na maslahi ya wachezaji Simba, Mkurugenzi timu ya mkoa wa Pwani vijana U-17 Copa Coca-Cola 2008.

Kuanzia mwaka 2008-2011, alikuwa

Katibu tawi la Simba Mpira Pesa Magomeni baadaye mwaka 2011 alichaguliwa kuwa Katibu tawi la Simba Vuvuzela hadi sasa.

Aliwahi kugombea Simba/TFF

Mwaka 2010, Mkoma aliwahi kugombea nafasi ya Ujumbe Wa Kamati ya Utendaji, aliombwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwaka 2011 huku akigombea tena nafasi ya

Ujumbe kamati ya utendaji Simba mwaka 2014 pamoja na nafasi ya Katibu mkuu Simba akiishia hatua ya 3 bora.