Huku Wasafi Festival, kule Fiesta haijawahi kutokea Bongo

Muktasari:

Wasanii mbalimbali wamethibitisha kushiriki Tamasha la Wasafi Festival ambao ni Navy Kenzo,Country Boy,Chin Beez na Nikki Mbishi huku wengine badpo hawajawataja wakati  kwenye Fiesta pia kuna wasanii mbalimbali ambao wameendelea kuzunguka katika mikoa tofauti linapofanyika tamasha hilo kama Nandy,Roma,Stamina,Maua Sama, Dogo Janja,Fid Q na Barnaba,

Hii ya Wasafi  na Clouds haijawahi kutokea kwani ni mwendo wa Bampa to Bampa mpaka kieleweke kama  msanii wa muziki wa kizazi kipya,Darasa alivyowahi kuimba.
Wakati Kampuni ya Clouds ikipanga  Tamasha lao kubwa la Fiesta kufanyika Dar es Salaam Novemba 24 huko kwa wapinzani wao wakubwa kampuni ya Wasafi nayo imepanga kufanya tamasha kubwa lijulikanayo kama Wasafi Festival  siku hiyo hiyo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.
Kampuni hizo mbili zimeingia katika vita kubwa ya kibiashsara kwani Clouds TV na Radio hazipigi nyimbo  za wasanii kutoka kampuni ya Wasafi inayoongozwa na Mkurugenzi Naseeb Abdul  maarufu kama Diamond Platnumz.
 Mameneja wa mwanamuziki huyo walishawahi kusema kuwa hawajali chombo chochote cha habari kutocheza nyimbo zao kwani wanajimudu wenyewe kutokana na nguvu kubwa waliyonayo kwa mashabiki.
Mashabiki wengi  wa muziki wana hamu ya kuona tamasha gani litafunika sikiu hiyo  kwani tayari tambo zimeanza kutoka kutoka kwa  watu wa pande zote mbili kila mmoja kilipromoti tamasha lake.
Diamond Platnumz alirusha jiwe gizani kwenye mtandao wake wa kijamii wa  Instagram kwa kuandika"24| 11| 2018 pale Nangwanda Sijaona  wakati Dunia ikishuhudia rasmi sanaa yetu pendwa inavyozaliwa pyaaaaaaaa baada ya mateso ya muda mreeefu....
#Sanaa imezaliwa upya
#Hawaamini wanacho kiona
jamani hii michezo ya Teaser #hizi kazi ni za watu
#Mchezo usiuchezee wewe
#kaaaaaaaaaaaaaaaabisa