Huko NBL Moto Utawaka

Saturday October 17 2020

 

By OliverAlbert

Ligi ya Taifa ya Mpira wa kikapu (NBL) inaanza kesho Oktoba 18-25  katika viwanja vya viwili, Don Bosco Upanga na Bandari Kurasini.
Mashindano hayo yatashirikisha timu 12 za wanaume na sita za wanawake.
Rais wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa amesema mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya DB Lioness itakayoikabili Ukonga Queens katika mchezo utakaoanza saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Don Bosco Upanga na utafuatiwa na mchezo wa wanaume kati ya JKT na Oilers.
Michezo hiyo itatanguliwa na mechi nyingine kati ya Vijana Queens dhidi ya Jeshi Stars saa 6:00 mchana, wanaume Savio watakaoonyeshana kazi na Rukwa Stars (saa 8:00 mchana) na Vijana itakayoumana na Ukonga Kings katika mchezo utakaoanza  saa 10:00 jioni.
Magesa amezitaja timu shiriki kuwa ni JKT, Oilers, Kurasini Heat na Arusha TCDC ambazo ziko kundi A wakati kundi B lina timu za Savio, ABC, Rukwa Stars na  Korogwe Heat.
Kundi C lina timu za Vijana City Bulls,Ukonga Kings, Pazi na Dodoma Panthers.
Magesa amezitaja timu shiriki kwa upande wa wanawake kuwa ni Vijana Queens, DonBosvo Lioness, Ukonga Queens, Jeshi Stars,Dodoma Queens na JKT Stars

Advertisement