Hizi hapa bato za Kombe la Ligi England

LONDON, ENGLAND. LIVER na Arsenal huenda zikakutana raundi ya nne tu ya Kombe la Ligi kufuatia droo iliyopangwa juzi, huku kukitarajiwa kuwapo na kipute cha London derby, Chelsea inaweza kukwaruzana Spurs. Kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa, Man United inaweza kuwa na shughuli dhidi ya ama Preston au Brighton kama itashinda mchezo dhidi ya Luton ugenini, Man City itahitaji kuwafunga Bournemouth kabla ya kumenyana na Millwall au Burnley. Liverpool itapaswa kuwafunga Lincoln City kupata fursa ya kucheza na Leicester City au Arsenal, huku Spurs itapaswa kuwachapa Leyton Orient na kupata nafasi ya kucheza na Chelsea, ambao itakuwa na kazi mbele ya Barnsley.Mechi zote zitapigwa Septemba 29 au Septemba 30.