Hispania vitani, UEFA Nation League

Muktasari:

Michuano hiyo ilianza mwaka jana  ambapo timu ya Taifa ya Ureno ndio ilifanikiwa kuchuakua kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Uholanzi bao 1-0  katika mchezo wa fainali

MADRID, HISPANIA. MICHUANO ya UEFA Nations League inatarajiwa kuendelea leo, ikiwa katika hatua ya makundi ambapo vinara wa kundi D kwenye ligi A, timu ya Taifa ya Hispania ikiwa nyumbani itashuka dimbani majira ya 3:45 usiku, kucheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Switzerland inayoburuza mkia katika dimba la Estadio Alfredo Di Stefano.

 

Switzerland inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi mbaya ya kupoteza michezo 15 kati ya 20 iliyokutana na Hispania huku minne ikiisha kwa sare na ikashinda mmoja tu.

 

Hispania ilikusanya alama nne baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ujerumani na ikaifunga Ukraine mabao 4-0 katika mchezo wa pili huku Switzerland ikiambulia alama moja baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ukraine mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ujerumani.Mchezo mwingine wa kundi hilo utakuwa kati ya Ujerumani inayoshika nafasi ya tatu dhidi ya Ukraine inayoshika nafasi ya pili.

 

Kundi C la ligi A, kutakuwa na michezo miwili ambapo Luxembourg itaumana na Cyprus saa 10:00 jioni, huku Montenegro ikicheza na Azerbaijan muda huo huo.

 

Pale Kundi C katika ligi hiyo hiyo kutakuwa na mchezo mkali wa Faroe Islands dhidi ya Latvia utakaochezwa saa 1:00 jioni na Andorra itakipiga na Malta saa 3:45 usiku.

 

Katika ligi B, kwenye kundi D vinara Liechtenstein watakuwa na kibarua mbele ya Gibraltar inayoshika nafasi ya pili, mchezo utapigwa majira ya 1:00 usiku.