UCHAMBUZI : Hili ndilo eneo linaloendelea kutawala soka la Afrika

Saturday November 3 2018Ali Mayay

Ali Mayay 

By Ali Mayay mayayt@yahoo.com

KATIKA mashindano ya Klabu Barani Afrika ambayo kwa sasa yapo katika hatua ya fainali tumeshuhudia timu kutoka nchi za Afrika ya Kaskazini zikiendelea kutawala soka la Afrika kwa upande wa Klabu, kitendo ambacho kinaendelea kuonyesha tofauti ya maendeleo ya soka kati ya nchi Afrika Kaskazini na nchi za maeneo mengine katika bara la Afrika.

Ukiangalia katika mashindano ya kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika ambayo kwa sasa ipo katika hatua ya fainali ,timu za El Ahly ya Misri na Eperance ya Tunisia zote zikiwa ni timu kutoka Kaskazini mwa bara la Afrika. Ukianza kuangalia kuanzia timu nane zilizoingia katika hatua ya robo fainali utaona picha halisi inayoonyesha tofauti hiyo ya maendeleo ya soka ninayoizungumzia.

Timu zilizoingia hatua ya robo fainali katika mashindano ya Klabu Bingwa kulikuwa na timu moja tu kutoka nchi za Afrika Magharibi ambayo ni Horoya FC kutoka Guinea, timu moja tu kutoka nchi za Afrika ya kati ambayo ni TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, timu moja tu kutoka Kusini mwa Afrika ya Primero de Agosto ya Angola huku timu nyingine zote tano zilizobakia katika hatua hiyo ya robo fainali zikiwa ni timu kutoka Kaskazini mwa Bara la Afrika. Timu hizo ni El Ahli ya Misri, ES Setif ya Algeria ,Waydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia na Etoile Du Sahel ya Tunisia.

Lakini baada ya hapo kati ya timu tano zilizoingia katika hatua ya Robo fainali kutoka nchi za Afrika ya Kaskazini, ni timu tatu kati yake zilifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali huku mbili kati yake zikiondolewa.

Zilizoingia hatua ya nusu fainli zilikuwa ni Al Ahli ya Misri, Es Setif ya Algeria na Esperance ya Tunisia zikiungana na Primero De Agosto ya Angola katika hatua hiyo.

Baada ya hapo timu zilizoingia hatua ya fainali zote ni za kutoka Kasakazini mwa bara la Afrika kwani Primero De Agosto ilitolewa na Esperance ya Tunisia katika hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi ya kwanza nyumbani kwao Angalo kwa bao 1-0 lakini ikakubali kufungwa 4-2 katika mechi ya marudiano iliyochezwa nchini Tunisia.

Hivyo Al Ahli na Esperance zote kutoka kaskazini mwa bara la Afrika zilifanikiwa kuingia hatua ya fainali .

Lakini ukiangalia pia katika mashindano ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika kuanzia katika hatua ya robo fainali utaona tena taswira inayofana na ile tuliyoiona katika Kombe la labu Bingwa kwani nusu ya timu zilizoingia katika hatua ya robo fainali zinatokea ukanda huo huo wa Kaskazini mwa bara la Afrika. Timu hizo ni Berkane ya Morocco,USM Algers ya Algeria,Raja Casablance ya Morocco na El Masrri ya Misri

Huku Afrika magharibi ikiwa na timu moja tu ya Enyimba kutoka Nigeria, Afrika ya kati ikiwakilishwa na timu mbili za Cara Brazaville kutoka Kongo Brazaville na AS vita kutoka jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, na timu ya mwisho ilikuwa ni Rayon Sport kutoka katika ukanda wetu wa nchi za Afrika ya Mashariki.

Baada ya hapo timu mbili tena kutoka Afrika Kasakazini za Raja Casablanca ya Morocco na Elmsri ya Misri zilifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali pamoja na Enyimba ya Afrika Magharibi na AS Vita kutoka Afrika ya Kati.

Lakini bado uwakilishi wa nchi za Afrika Kaskazini ukaendelea tena kutamalaki kwani timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali ni Raja Casablanca kutoka Morocoo na AS Vita kutoka Jamhuri ya Kidemkrasi ya Kongo ambapo michezo miwili ya fainali inatarajiwa mmoja kuchezwa mwisho mwa mwezi huu (Novemba) huku mechi ya pili ikirarajiwa kuchezwa mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Hivyo uwaklishi huo wa Klabu kutoka nchi za Afrika Kaskazini unaendelea kuonesha tofauti ya maendeleo ya soka katika ngazi ya vilabu kwani vilabu kutoka nchi za Morocco, Tunisia, Algeria na Misri vinaendelea kuweka historia ambayo inavifanya kuwa vikubwa kila siku kwani siku zote wasifu wa timu ukiachilia mbali ukongwe wa timu lakini hupimwa kutoka na mafanikio ambayo timu husika imewahi kuyapata.

Hivvyo kufanya vizuri kwa Klabu kila mara tena kwenye mashindano makubwa kama haya ya Afrika bila shaka hiyo wataendelea kukuza wasifu ambao utavitofautisha na klabu kutoka katika mataifa mengine kama vile Ukanda wa Afrika ya kati, mashariki, Kusini na Magharibi.

Ni vyema mashirikisho ya katika maeneo mengine yakaja na mikakati ya pamoja kwa upande wa vilabu ili kuinua soka kwa maeneo kama walivyoanza katika mashindano ya Under -17 ya CAF.

Kwa leo naomba kushia hapo huku nikisubiri mrejesho kutoka kwako !

Advertisement