Henry, Vieira watunziana heshima

Muktasari:

  • Matokeo hayo yameifanya Monaco kujiondoa hatua moja kutoka mkiani wa Ligi Kuu, huku Nice ikiwa nafasi ya sita.

Paris, Ufaransa. Kwa mara ya kwanza wamekutana wakiwa makocha Thierry Henry wa Monaco na Patrick Vieira wa Nice watunziana heshima baada ya timu zao kutoka sare 1-1.

Allan Saint-Maximin alifunga bao la kuongoza kwa Nice akimalizia makosa ya Youssef Ait Bennasser, lakini wageni hao walipata pigo baada ya mchezaji wao Ihsan Sacko kutolewa nje kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko.

Monaco ikiwa na faida ya mtu mmoja ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia Benoit Badiashile kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Saint-Maximin had a penalty saved and Monaco's Radamel Falcao hit the post.

Vieira ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England akiwa na Arsenal wakati Henry ametwaa  mara mbili, wawili hao walikuwa na mchango mkubwa msimu wa 2003-04 ambao Arsenal iliweka rekodi ya kutwaa ubingwa bila ya kufungwa.

Pia wawili hao waliisaidia Ufaransa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 1998 pamoja na lile la Mataifa ya Ulaya 2000.