Hee Fei Toto bado yupoyupo sana bongo

Muktasari:

Kiungo Fei Toto kwa sasa ni mapema kwake kuondoka nchini na kwenda kucheza soka nje, anasubiri hadi pale kiwango chake kitakapoimalika zaidi.

Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema bado anahitaji muda mwingi zaidi kufikia kiwango cha kuondoka Tanzania na kwenda kujaribu soka la kulipwa nje ya nchi.

Fei Toto alisema anatamani kutoka Tanzania, lakini kiwango alichonacho sasa bado hakimridhishi na kumfanya akawa na haraka ya kujaribu kucheza soka nje.

Alisema umri bado unamruhusu kuendelea kupambana zaidi na kuimaiisha uwezo wake ambao ndio utakaomfanya aweze kuwa na uamuzi utakao kuwa na faida zaidi kwake na Tanzania kwa ujumla.

"Kwa sasa naweza kusema tayari nimeanza kumudu uchezwaji wa soka la ushindani, lakini bado sijafikia kiwango ambacho kinaweza kunitoa hapa nilipo na kunipeleka nchi nyingine na nikaweza kumudu kiurahisi muda ukifika nitatafuta njia nyingine itakayoitoa hapa na kunifikisha kimataifa,"

"Silewi sifa ninazopewa naendelea kupambana zaidi kubwa ninaloliangalia ni kukikuza kipaji changu ili niweze kucheza sehemu yoyote nitakayokwenda kucheza," alisema Fei Toto.