Hawa nitarejea aja na wimbo mpya wa nacheka

Tuesday August 6 2019

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Mwimbaji wa Hawa Said ‘Hawa nitarejea’ aliyeshirikishwa na Diamond Platinumz ametoa wimbo wa ‘Nacheka’ baada ya kupona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Hawa ambaye aliwahi kukiri kuwa amegeuka kuwa muathirika mkubwa wa pombe haramu aina ya gongo huku akiomba msaada aweze kuachana na ulevi wa kupindukia.

Mwanamuziki Diamond alijitolea kumpeleka India kwa ajili ya matibabu amesema ameamua kutoa wimbo huo uliombatana na video ni moja ya zawadi kwa watanzania kutokana na uvumilivu walioufanya akiwa amejihusisha na kitendo kichafu.

“Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyezi mungu na pili mwanamuziki Diamond kwa kuweza kunipeleka India kwa ajili ya matibabu, bila kuwasahau watanzania wote waliokuwa sambamba na mimi pindi nilipopotea kwa utumiaji wa pombe aina ya gongo na kunisababishia tatizo la moyo,na hata nilivyokuwa naumwa na ndio maana nimeona bora niwape zawadi ya wimbo wa kucheka ambayo unaelezea historia ya maisha yangu,” alisema Hawa.

Aidha hawa ameiambia MCL Digital kuwa, kujikubali na uvumilivu pamoja na kumuomba Mungu ndio vimemfanya leo hii kuliona tabasamu lake na amehaidi mashabiki zake kuwaletea kazi nzuri katika burudani muziki anayoifanya.

 

Advertisement

 

Advertisement