Havertz kuikamua mapesa Liverpool

Muktasari:

Kiungo huyo mwenye miaka 20, amekuwa na msimu mzuri Ujerumani. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anamtaka Havertz katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

London, England. Liverpool imekubali kuvunja benki kutoa Pauni 107 kunasa saini ya nyota wa Bayer Leverkusen Kai Havertz.

Klabu hiyo imepanga kuingia vitani kuwania saini ya mchezaji huyo ikiwa na hofu dhidi ya miamba mingine Manchester United, Barcelona na Bayern Munich zinazomtaka.

Kiungo huyo mwenye miaka 20, amekuwa na msimu mzuri Ujerumani. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anamtaka Havertz katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Havertz amekuwa chachu ya mafanikio Leverkusen ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi za mwisho mara 21 na kuweka timu hiyo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani.

Kwa ujumla Havertz amefunga mabao 31 na kutoa pasi za mwisho mara 23 katika mechi 126 tangu akiwa kinda wa miaka 17 Leverkusen.

Mchezaji huyo alikuwa sehemu ya timu ya taifa chini ya kocha Joachim Low na amefunga bao katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Argentina Oktoba.