Haruna Chanongo ashindwa kuvumilia mziki wa Mawenzi

Wednesday September 12 2018

 

By Juma Mtanda

 Morogoro. Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila ametoa mchongo kwa Mawenzi

Market FC kama inataka kufanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza msimu huu na

kutinga Ligi Kuu Bara msimu ujao huku kiungo wake, Haruna Chanongo akikazia.

Katwila amesema ili Mawenzi iweze kufanya vizuri katika michezo yao ya Ligi Daraja

la Kwanza msimu huu, wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja kuanzia benchi la

ufundi, wachezaji na uongozi.

Katwila amesema,  Mawenzi imefanikiwa kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 dakika za mapema

na kuhimili kasi na mikiki ya Mtibwa waliocheza nayo mechi ya kirafiki Uwanja wa

Jamhuri Morogoro Jumatatu iliyopita.

“Mawenzi wamecheza mchezo nzuri dhidi yetu na kufanikiwa kutufunga bao 1-0,

wamehimili kasi na maarifa ya wachezaji wangu, jambo wanapaswa kuliendeleza katika

michezo yao ya Ligi Daraja la Kwanza.”alisema Katwila.

Naye kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo alisema, anaiona Mawenzi 

tofauti na msimu uliopita na endapo viongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro na

ule wa klabu wakishirikiana watafikisha malengo.

“Nimeiona Mawenzi ile ya msimu uliopita na huu. Hii ya sasa inaweza kutimiza malengo

endapo tu uongozi na wachezaji wakashirikiana,”alisema Chanongo.

Mashabiki waendelee kuwaunga mkono wachezaji na wasiwakatishe tamaa kwani ameona

Mawenzi ikicheza kwa nguvu na uelewano ingawa wanapaswa kuongeza kasi ili kuweza

kuwachanganya maadui zao,"alisema Chanongo.

Kocha mkuu wa Mawenzi, Mussa Rashid alisema, timu yake inahitaji kucheza michezo ya

kirafiki 12 kabla ya kuanza ya ligi na wataanza kutupa karata yao kwa kwa Mufindi FC

Septemba 29, katika uwanja wa jamhuri Morogoro.

Rashid alisema, kwa sasa anatafuta kucheza michezo miwili ya kirafiki baada ya

kucheza 10, kwani itamsaidia kupata mwelekeo wa kupata kikosi bora chenye ushindani

ili kupata matokeo mazuri ya kusaka nafasi ya ligi kuu msimu ujao.

Advertisement