Harmonize kuipeleka singeli kimataifa

Sunday February 9 2020

 

By RHOBI CHACHA

BAADA ya kutoa nyimbo tatu mfululizo tangu ajitoe Lebo ya WCB Wasafi, nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamornize amefyatua ngoma nyingine mpya iitwayo'Hujanikomoa' ya mahadhi ya Singeli.
Staa huyo wa Uno, Kushoto Kulia na Hainistui, alisema ngoma hiyo ni katika kuthibitisha yupo fiti katika kila miondoko ndio maaana safari hii kaachia ngoma hiyo iliyoanza kukimbiza hewani.
Wimbo huo umewekwa jana Jumamosi na hadi leo saa 5:03 asubuhi imetazamwa na watu 233,097 na kupata like 9,183.
Baadhi ya mistari ya wimbo huo wa Hujanikomoa inasema;  ”Mwambieni dada yenu hajanikomoa...  eti badala ya kujenga anabomoa... eti mapenzi hayalazimishwi, tena ni siri ya watu wawili...wala sikuwa mbishi alivyonikataa kimwili...Asa jana niko kwa mama wini...napiga zangu chai vitumbua.. eti kasambaza za chinichini ..mie bado nina msumbua..oooh mwambie dada yenu hajanikomoaaa..'
Singelin kwa sasa inaonekana kuwaumizwa kichwa wakali wengi wa Hip Hop na Bongofleva baada ya mkongwe Professor Jay mwaka juzi naye kuachia  ‘Kazi Kazi’ aliomshirikisha Sholo Mwamba na kuamua kuuita style hiyo jina la Hip Hop Singeli.
Pia staa mwingine wa kimataifa, Diamond Platnumz aliachia ngoma iitwayo Platnumz-Moto aliyoshirikishwa, huku Shetta naye akifuata mkumbo na ' Uswahilini’ amemshirikisha mkali wa muziki huyo Tanzania ‘Mzee wa Bwax’.

Advertisement