Harmonize ‘nyuma ya pazia’ katika ngome ya Wasafi

Muktasari:

Hata hivyo, chanzo cha habari cha kuaminika kiilicho karibu na Hamornize kimesema sababu kuu ya kujiondoa katika Lebo hiyo ni mchumba wake Sarah kumpa jeuri ya fedha na kumfungulia Miradi ukiachilia mbali ule wa kumiliki studio yake ya muziki liyopo Sinza Kijiweni, pamoja na kumjengea ghorofa maeneo ya Mbezi beach jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam.Huenda ukawa na maswali mengi kuhusu hatma ya Hamonize katika ngome ya Wasafi baada ya kuwepo kwa fukuto lililodumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa kuwa anajitoa.  

Msanii huyo wa kwanza kudondosha saini ya kuhudumu katika ngome hiyo miaka minne iliyopita, ambapo lebo hiyo iliyo chini ya staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz imekuwa ikisimamia kazi zake za muziki ikiwemo shoo za ndani na nje ya nchi, video, kolabo za kitaifa na kimataifa na mikataba mbalimbali ambapo vyote hivyo vimemfanya kuwa msanii mwenye mafanikio ya haraka kwa sasa kwenye muziki huo.

Sasa rasmi milango yake iko wazi kuondoka baada ya Meneja wa kundi la Wasafi, Sallam Sk kuthibitisha katika kituo cha televisheni ya Wasafi.

“Harmonize moyo wake haupo Wasafi, lakini ukweli ni kuwa bado ana mkataba na kundi hilo, ameshatuma barua ya maombi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote,” alisema Sallam.

“Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali.

Hata hivyo, chanzo cha habari cha kuaminika kiilicho karibu na Hamornize kimesema sababu kuu ya kujiondoa katika Lebo hiyo ni mchumba wake Sarah kumpa jeuri ya fedha na kumfungulia Miradi ukiachilia mbali ule wa kumiliki studio yake ya muziki liyopo Sinza Kijiweni, pamoja na kumjengea ghorofa maeneo ya Mbezi beach jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na madai hayo na kauli ya Sallam Sk kuweka wazi suala la Hamornize, wapo baadhi ya watu wanadai tukio hilo linaweza kumgusa mwanamuziki wa bongo Fleva Ali Kiba, kwa kile kupotezwa katika ushindani na Diamond sasa itakuwa ni Diamond na Hamornize.

Jitihada za kumtafuta Hamornize ili kuweza sawa suala hili hazikufanikiwa kwa kuwa namba zake zote mbili za simu kutokuwa hewani.