Hans Poppe aachiwa kwa dhamana

Tuesday October 16 2018

 

By Omar Fungo

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zakaria Hans Poppe achiwa kwa dhamana ya Sh 15milioni kesi kutajwa Ijumaa.

Hans Poppe alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo, saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani

Awali upande wa Mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro aliomba kuunganisha Hanspope katika kesi inayowakabili aliyekuwa rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu.

Hata hivyo, wakili wa Utetezi ukiongozwa Wandiba alipinga akidai kuwa mahakama ilishatoa uamuzi kuwa kesi iendelee kwa washtakiwa waliopo Mahakamani na kwamba kwa maombi hayo, mahakama inalengo la kirudisha nyuma kesi hiyo.

Hivyo, Wandiba ameomba Mahakama hiyo iendelee na kesi dhidi ya washtakiwa waliopo Mahakamani na Hanspoppe afunguliwe mashtaka yake.

Hakimu Mkazi Mkuu anayeshikiliza shauri hilo, Thomas Simba, baada ya kusikiliza hoja za pande zote, anandika uamuzi ama kukabiliana na upande wa mashtaka wa kumuunganisha Hanspoppe katika kesi ya akina Aveva au kutupilia mbali maombi hayo ya upande wa mashtaka.

Hanspope amefikishwa katika Mahakama hiyo, saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.

Habari zaidi zinakuja kuhusu kesi hii utazipata hapa

Advertisement