HARRY Kane aambiwa apigwe kisu

Sunday April 14 2019

LONDON, ENGLAND

STRAIKA, Harry Kane ameambiwa njia pekee ya kumaliza matatizo yake ya mara kwa mara ya maumivu ya enka ni kufanyiwa upasuaji.

Staa huyo wa Tottenham anaamini atakuwa fiti kuichezea England kwenye nusu fainali ya Nations League dhidi ya Uholanzi itakayopigwa Juni 6 baada ya sasa kuumia enka kwa mara ya tangu ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Kwa hali ya mambo ilivyo, Kane haonekani kama atacheza tena kwenye kikosi cha Spurs msimu huu huku mtalaamu wa upasuaji, Mark Davies akiamini kumfanyia upasuaji staa huyo ndiyo suluhisho la kudumu.

“Nadhani kwa sasa ninachokifikiria ni kwamba wangemfanyia upasuaji tu ili kumaliza tatizo lake. Ningeweza kuzungumza naye kumwelezea umuhimu wa kufanya upasuaji,” alisema daktari Davies.

Kane amekuwa akisitasita kufanya upasuaji akihofia kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi huku akikwepa kufanya jambo hilo akiwa na matumaini kwamba huenda Spurs ikafika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na yeye akifanyiwa upasuaji sasa badi anaweza kukosa mechi hiyo. Lakini, Davies alisema ndio njia pekee ya kumaliza tatizo lake la sivyo atakuwa mtu wa kurudi uwanjani na kuuumia tena.

Advertisement