Gyan achoka,akimbilia mahakamani

Muktasari:

Sababu za Gyan kuomba talaka zinadaiwa anashuku ikiwa yeye ndiye baba halisi wa watoto wake wote hao watatu.

STRAIKA wa Ghana, Asamoah Gyan karipotiwa kuwasilisha kesi mahakamani akiomba kumtaliki mke wake, Gify Gyan.

Ombi hilo aliliwasilisha katika mahakama ya kifamilia jijini Acrra. Gyan na Gify wamekuwa wapenzi tangu mwaka 2003 na walifunga ndoa 2013 ikiwa ni miaka mitano iliyopita baada ya kujaliwa mtoto wao wa pili na kwa jumla wana watoto watatu.

Sababu za Gyan kuomba talaka zinadaiwa anashuku ikiwa yeye ndiye baba halisi wa watoto wake wote hao watatu.

Kando na kuwasilisha maomba ya talaka, vilevile Gyan anataka watoto hao wafanyiwe vipimo vya DNA kuthibitisha ikiwa kama kweli yeye ndiye baba yao.