Gwambina, Ihefu zapewa tano

Muktasari:

Pamoja na kuzishukuru timu hizo kuzipongeza alizigeukia Simba, Yanga na Coastal Union kwamba hawezi kuzipongeza kwani zilipaswa kumiliki viwanja tangu miaka ya nyuma.

Katika hotuba ya  rais wa TFF,  Karia amegusia suala la timu kuwa na viwanja vya mazoezi na kuzipongeza Gwambina FC na  Ihefu kuwa na viwanja.
Amesema timu hizo kumiliki viwanja ni hatua kubwa ya maendeleo ya soka nchini, akizitaka timu za ligi ya VPL kuzingatia Hilo.
"Wanastahili pongezi na ziwe mfano kwa timu nyingine ambazo hazina viwanja,"anasema.
Pamoja na kuzishukuru timu hizo kuzipongeza alizigeukia Simba, Yanga na Coastal Union kwamba hawezi kuzipongeza kwani zilipaswa kumiliki viwanja tangu miaka ya nyuma.
"Simba na Yanga zilipaswa kuwa na viwanja tangu miaka ya 70, lakini pia Mtibwa Sugar kiwanja chao kina miaka 24 hakijaboreshwa vitu vingi, yafanyiwe kazi maana vitafungiwa,"anasema.
Mbali na viwanja amezitaka timu za ligi kuu na madaraja ya chini kuwa timu za U-17 na 20 zitakazokuwa zinaandaa vijana ambao watakuwa msaada kwenye timu ya Taifa.
"Hasa timu za ligi kuu nawasisitiza kuwa na timu za U- 17 na 20 kwani ndizo zinazokuwa zinaandaa vijana wetu kupata uzoefu" amesema.