Advertisement

Gundogan agoma kwenda Barca

Gundogan amebakiza mkataba wa miaka miwili Etihad na Barcelona walionyesha nia na dhamira ya dhati kabisa kuhitaji saini yake

IN SUMMARY

Gundogan amebakiza mkataba wa miaka miwili Etihad na Barcelona walionyesha nia na

dhamira ya dhati kabisa kuhitaji saini yake akatue kwenye kikosi chao huko Nou Camp.

Advertisement

 Staa wa Manchester City, Ilkay Gundogan amesema amegomea ofa ya kwenda kujiunga na

Barcelona ili aendelee kubaki kwenye kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu England huko

Etihad.

Gundogan amebakiza mkataba wa miaka miwili Etihad na Barcelona walionyesha nia na

dhamira ya dhati kabisa kuhitaji saini yake akatue kwenye kikosi chao huko Nou Camp.

Mjerumani huyo akili yake kwa sasa ni kusaini mkataba mpya Man City ili kufuta

kabisa ndoto za Barcelona wanaomtaka kwenye kikosi chao. Klabu nyingine inayomtaka

Gundogan ni AC Milan ya Italia.

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept