Guinea, Nigeria hapatoshi nusu fainali Afcon

Muktasari:

  • Mchezo wa Guinea dhidi ya Nigeria unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timuz zote kusifika kwa kucheza soka safi.

Dar es Salaam. Kocha wa Guinea, Camara Mohammed ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Nigeria utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Camara alisema walipambana na timu ngumu tangu mwanzo wa fainali, hivyo hawatarajii kuona wakitoka badala yake kuingia fainali.

"Tumekutana na timu ngumu katika kundi letu, lakini tulifanikiwa kuzitoa, kwahiyo mchezo wetu dhidi ya Nigeria tunataka kushinda ili kutinga katika hatua ya fainali," alisema Camara.

Aliongeza mchezo wao dhidi ya Nigeria ugakuwa mzuri kutokana na kutambua timu zote zinazokutana ni bora.

Wakati huo huo kocha msaidizi wa Nigeria, Olantusi Baruwa alisema wamekuja katika fainali za Afcon wakiwa na lengo la kufuzu katika kombe la Dunia na kufika katika hatua nzuri ya Fainali za Afcon.

"Tunataka ubingwa kwa muda huu baada ya kufuzu katika Kombe la Dunia, naamini kabisa vijana wangu watapambana mpaka mwisho kuhakikisha hili linawezekana," alisema Baruwa.