Guendouzi afurahia maisha Arsenal

Wednesday September 12 2018

 

 Kiungo mpya wa Arsenal, Matteo Guendouzi amesema ni kama anaota njozi ya mchana kwa kile kinachomtokea msimu huu.

Guendouzi ameihama timu ya Daraja la Pili, Lorient ya huko Ufaransa na kwenda kujiunga Arsenal kwenye dirisha lililopita na tangu atue Emirates, panga pangua amekuwa kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Unai Emery.

Kiungo huyo kinda alisema kwa sasa anaishi ndoto zake kwa namna alivyopokewa na wachezaji wenzake na benchi la ufundi huko Emirates.

Advertisement