Guardiola atakiwa Man United

Sunday September 9 2018

 

Nyota wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona ameweka wazi kwamba anatamani Pep Guardiola ndiye angekuwa anaendesha jeshi la Old Trafford.

Cantona ameweka wazi kwamba hafurahii soka la Manchester United chini ya kocha wa sasa Jose Mourinho na kama ingekuwa Guardiola ndiye kocha, mambo yangekuwa poa.

"Ukweli ni kwamba soka la Manchester United si zuri, lakini bado tupo kwenye hatua za awali za msimu, ngoja tuone labda mambo yatabadilika. Naamini watapata kombe, naamini hivyo,”

"Lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba wanacheza vibaya, kocha hawaonyeshi njia nzuri ya kucheza ili kupata matunda.

"Hakuna ubunifu wa aina yoyote, Mourinho ni kocha mzuri lakini si kwa Manchester United. Nadhani Manchester United ingempata Guardiola mambo yangekuwa mazuri sana. Kwa sasa anafanya maajabu akiwa na Manchester City, ni kocha wa kiwango cha Man United.”

Advertisement