Guardiola amchimba mkwara Leroy Sane

Muktasari:

City wamepanga kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani dau la pauni 90 milioni na wakati bado Bayern bado haijahafiki dau hilo, Sane mwenyewe ameshindwa kuweka wazi kama anavutika na mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao.

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amempiga mkwara winga wa klabu hiyo, Leroy Sane kwa kudai kama staa huyo hana furaha basi anaruhusiwa kuondoka klabuni hapo wakati huu akisakwa na klabu ya Bayern Munich.

City wamepanga kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani dau la pauni 90 milioni na wakati bado Bayern bado haijahafiki dau hilo, Sane mwenyewe ameshindwa kuweka wazi kama anavutika na mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao.

Mpaka sasa hajasaini mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa ukiwa umebakiza miaka miwili na vigogo wa Bayern Munich wameripotiwa mara nyingi kukiri kumtaka staa huyo kwa ajili ya kuziba mapengo ya Arjen Robben na Franck Ribery ambao wameondoka klabuni hapo.

Sane ameichezea Manchester City jumla ya mechi 89 na kuifungia mabao 25 hadi sasa.