Guardiola afichua majanga yalimponza kwa Madrid

Muktasari:

  • Ilikuwa ni kubadili misamiati tu, kimsingi nilimaanisha tukicheza vizuri tutapoteza mechi chache, natumaini kuwa na wachezaji ambao watakuwa vizuri katika kipindi chote cha mwaka ili niwe na wachezaji wengi wa akiba na hivyo tutajihakikishia kucheza vizuri na kuendelea kushinda.

TOLEO lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, tuliona namna ambavyo Mwandishi Marti Perarnau aliendelea na mahojiano yake na Kocha Pep Guadiola na moja ya swali alilomuuliza ni iwapo wachezaji wa Bayern walikuwa wakimuunga mkono kocha huyo katika juhudi zake kwenye timu. Sasa endelea…

Pep: Kimisngi nashukuru kwa juhudi zote zilizofanywa na wachezaji ambao walijikuta katika wakati mgumu kutokana na staili hii ya uchezaji, staili ambayo ilikuwa haiendani na aina ya uchezaji wao, nafikiri wote bila kujali kama waliichukulia kirahisi rahisi lakini pia waliona umuhimu wa uchezaji wetu wa kuzingatia maeneo pamoja na mbinu na msisitizo wa kukimbia uwanjani kwa malengo maalumu na si kukimbia tu.

“Siwezi kuamini kama kuna mmoja wao ambaye anaweza asiipende aina hii ya kazi tuliyoifanya, na kumbuka haikuwa rahisi kwa wachezaji kutoka kushinda mataji matatu makubwa msimu uliotangulia na kuendelea kuwa fiti kiakili na kimwili.

Perarnau: Je, haikatishi tamaa kucheza soka la kushambulia huku ukifahamu shambulizi moja tu la kushitukiza linaweza kuivuruga kazi yenu yote?

Pep: Ndio, hilo ni kweli lakini pia inaridhisha pale mnapozuia mashambulizi ya kushitukiza ya wapinzani wenu. Jambo moja la msingi la kuliweka wazi ni ukweli unaposhambulia vizuri katika aina hii ya uchezaji unakuwa umejilinda na kuupoteza mpira mahali popote au kwa namna yoyote inavyoweza kutokea.

“Hilo lilikuwa kosa letu kubwa lililotusababishia majanga ya Madrid, niliweza kuliona hilo tangu mwanzo lakini ilikuwa vigumu kubadili mfumo ghafla na nililazimika kusubiri hadi wakati wa mapumziko lakini hadi hapo ikawa tayari tumechelewa.

“Nilibadili mfumo kipindi cha pili na kuanza kuutumia wa 4-3-3 na katika kipindi cha pili tatizo hilo halikujitokeza tena na hatukupata matatizo ya mashambulizi ya kushitukiza.

“Kwa Ujerumani wachezaji wamezoea kucheza kwa kutumia nafasi, angalia goli letu la pili katika fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Dortmund, Muller kwa mfano alikuwa na eneo ambalo analipenda lakini ili kutengeneza nafasi katika eneo hilo wakati mwingine ni lazima ushuke nyuma.

“Na hiyo ni kwa sababu kama una wapinzani ambao wamejazana katika eneo lao la penalti na hapo hakutakuwa tena na nafasi na kazi itakuwa ngumu zaidi kuwaweka katika wakati mgumu.

Perarnau: Miezi michache iliyopita uliniambia mtacheza vizuri msimu ujao lakini mtapoteza mechi nyingi zaidi, hili likoje?.

Pep: Ilikuwa ni kubadili misamiati tu, kimsingi nilimaanisha tukicheza vizuri tutapoteza mechi chache, natumaini kuwa na wachezaji ambao watakuwa vizuri katika kipindi chote cha mwaka ili niwe na wachezaji wengi wa akiba na hivyo tutajihakikishia kucheza vizuri na kuendelea kushinda.

“Nafikiri tutacheza vizuri si hatutajilinganishi na Kocha Jupp (Heynckes) na mafanikio yake ya mataji matatu kwa msimu, badala yake kucheza huko vizuri ni kutokana na mafanikio yetu ya msimu huu.

“Ni jambo la kawaida baada ya mafanikio yote ya Jupp kila mtu alishangaa ni kwa nini tulihitaji kufanya mabadiliko, kuna wakati hata mimi nilikuwa nafikiria hivyo hivyo.

Perarnau: Kuna hoja kwamba ni muhimu kufanya mabadiliko baada ya mataji matatu kwa sababu katika soka usipobadili mambo utakwama, hili unalizungumziaje?

Pep: Najaribu kufikiri tu mambo yangekuwaje iwapo tusingefanya mabadiliko, lakini soka linahusu mambo ya mabadiliko hutakiwa kuwa hivyo hivyo, na mabadiliko yenye kuleta mafanikio yanategemea zaidi na aina ya wachezaji ulionao.

“Nililazimika kutumia staili ambayo sijajitoa katika kuitumia mara kwa mara kwa msimu huu (2013/14) lakini mabadiliko yalidhamiria kuwafanya wachezaji wapate wepesi katika mechi na kuwa na ari na kasi mpya.

“Unahitaji kufanya makosa kama una nia ya kupiga hatua, na unahitaji kuwajua wapinzani wako pamoja na aina ya ligi unayoshiriki, hadi sasa tayari nimeshacheza na wapinzani wote wa hapa, navijua viwanja vyao, makocha na naijua na kuielewa klabu.

Itaendelea Jumamosi ijayo…