Advertisement

Gor Mahia, Everton mechi yao kimeeleweka!

Mtanange wa kukata na shoka ambao unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka Afrika mashariki na kati, kati ya mabingwa wa soka nchini Kenya, Gor Mahia dhidi ya Everton ya England, sasa itachezwa mwezi Novemba, katika Uwanja wa Goodison Park, nchini England.

 

BY Fadhili Athumani

IN SUMMARY

  • Kwa mujibu wa waandaaji wa mechi hiyo ya kirafiki, itakayofanyika Jijini Liverpool, nchini Uingereza, kampuni ya kubeti ya Sportpesa ni kwamba, mtanange huo utapigwa kati ya Novemba 6 na 7, na mshindi ataibuka na Kombe la heshima la Sportpesa. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Gor Mahia, katika ardhi ya Malkia.

Advertisement

Nairobi, Kenya. Mtanange wa kukata na shoka ambao unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka Afrika mashariki na kati, kati ya mabingwa wa soka nchini Kenya, Gor Mahia dhidi ya Everton ya England, sasa itachezwa mwezi Novemba, katika Uwanja wa Goodison Park, nchini England.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mechi hiyo ya kirafiki, itakayofanyika Jijini Liverpool, nchini Uingereza, kampuni ya kubeti ya Sportpesa ni kwamba, mtanange huo utapigwa kati ya Novemba 6 na 7, na mshindi ataibuka na Kombe la heshima la Sportpesa. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Gor Mahia, katika ardhi ya Malkia.

Akizungumzia mechi hiyo, Kocha mkuu wa Gor Mahia, Dylan Kerr, ambaye timu yake inahitaji kushinda mechi tatu tu kutetea ubingwa wao, alisema: "Hii ni fursa adhimu sana kwangu, tunajiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo, naamini hadi kufikia Novemba tutakuwa tayari tumebeba ndoo."

Mkurugenzi wa SportPesa, Captain Ronald Karauri, alisema ziara hiyo itawapa wachezaji wa Gor Mahia fursa ya kutembelea moja ya viwanja kongwe nchini England na kuongeza kuwa Everton ni moja ya klabu Kongwe kwenye EPL kwa hiyo kucheza nao ni heshima kwa. 

 

 

Kogalo walipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kutetea ubingwa wa Kombr la Sportpesa kwa kuifunga Simba ya Tanzania, katika makala ya pili ya Kombe hilo, yaliyofanyika Juni 3-10 huko Nakuru na kushirikisha vilabu nane kutoka Afrika Mashariki.

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept