Gidabuday:Tulieni kila kitu ni fedha mjue

Muktasari:

  • RT si unafahamu kama kesho Ijumaa watafanya mashindano ya wazi ya Taifa yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha?.

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday buana amewasikia baadhi ya wadau waliokuwa wakihoji kuhusu mashindano ya wazi ya Taifa akaamua kuwajibu hivi.

RT si unafahamu kama kesho Ijumaa watafanya mashindano ya wazi ya Taifa yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha?.

Sasa buana tofauti na ilivyozoeleka kwenye mashindano ya Taifa timu shiriki kugharamiwa chakula na malazi, msimu huu kila mwanariadha anajigharamia mwenyewe huku idadi ya michezo ikipunguzwa na mashindano yakifanyika kwa siku moja.

Kitendo ambacho kilipondwa na baadhi ya wadau, lakini RT kupitia kwa Katibu wake Mkuu wala haikutaka kuwanyamazia kimya.

“Taarifa za wanaohoji kuhusu mashindano yetu, tunazo ila wala hawatusumbui, niwambie tu, kila kitu ni pesa na hapa ndipo uzalendo wa riadha utaonekana kuanzia hapo na wala sio kitu kingine.

“Ni mashindano gani ya Taifa kuna zawadi ya fedha kwa washindi, lakini sisi tumeamua kutoa motisha hiyo kwa washindi katika kila mchezo wa riadha kwenye mashindano haya, holo nalo hawajaliona bali wanahoji vitu vingine,” alisema Gidabuday.