Gaucho kufanya maajabu ligi ya wanawake

Friday November 29 2019

Gaucho- kufanya- maajabu- ligi ya wanawake-MSHAMBULIAJI - Simba Queens-Tanzania Bara-mwanahamisi-Omary-

 

By Olipa Assa

MSHAMBULIAJI wa Simba Queens, Mwanahamisi Omary 'Gaucho' amesema atatumia baadhi ya mbinu alizopata kwenye michuano ya Chalenji, kuisaidia timu yake kufanya maajabu Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea Desemba 7, timu yake itashuka dimbani na JKT Queens jambo analoamini watashinda mchezo huo.
Anasema katika michuano ya Cecafa amejifunza mbinu nyingi dhidi ya timu walizokuwa wanashindana nazo, kubwa ni namna ya kuthamini majukumu yao.
"Baadhi ya ufundi niliouona kwenye michuano ya Cecafa, naamini utanifaa nikiuhamishia kwenye ligi yetu, naamini nitafanya kitu,"
"Soka la wanawake kwa sasa limekuwa na mvuto, nilisikia faraja kuona namna ambavyo mashabiki walijitokeza kutuunga mkono kwenye michuano ya Cecafa, hii inanifanya nijitume zaidi,"anasema.

Advertisement