Ferdinand afichua siri ya Arsenal, ni Torreira

Tuesday November 6 2018

LONDON, ENGLAND. ARSENAL wanachekelea wanachokiona kwa sasa katika timu yao. Lakini Rio Ferdinand, mlinzi wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England amedai kwamba anajua sababu ya msingi ambayo inawafanya Arsenal wachekelee.

Jumamosi jioni, Arsenal walionyesha kiwango bora katika pambano la Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool ambalo walitazamiwa kufanya vibaya kutokana na ukali wa Liverpool licha ya siku za karibuni kushinda mechi nyingi mfululizo.

Ferdinand anaamini kwamba licha ya wachezaji wengi wa Arsenal kuwa vizuri lakini ni mchezaji mmoja tu ndiye ambaye amesababisha kwa kiwango kikubwa mambo kwenda sawa pale Arsenal. Lucas Torreira, staa wa kimataifa wa Uruguay.

Torreira ambaye ni mfupi kwa kimo, alinunuliwa kwa dau la pauni 25 milioni kutoka Sampdoria ya Italia katika dirisha kubwa lililopita mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Russia ambako alikuwa akiiwakilisha Russia.

Amekuwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha Arsenal kwa sasa na katika pambano dhidi ya Liverpool, Torreira alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Arsenal haijapoteza pambano lolote katika mechi ambao yeye ameanza msiu huu.

Ferdinand anaamini kwamba staa huyo ndiye chachu ya kila kitu katika kikosi cha Arsenal na kwa muda mrefu walikuwa wakikosa mchezaji wa aina yake katika kikosi cha Arsenal ambacho kilikuwa kinasuasua katika utawala wa kocha aliyepita, Arsene Wenger.

“Kitu kikubwa kwa Torreira ni kwamba anaijua nafasi yake. Arsenal wameleta wachezaji wengi katika nafasi yake kwa miaka mingi lakini wote walichemsha. Torreira ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kuifungua safu ya ulinzi kwa pasi. Atacheza pasi fupi kwa ajili ya kuiendesha timu.” alisema Rio.

“anataka kuchukua mpira ili kuwawezesha wachezaji wengine kama akina Mesut Ozil kucheza. Anaweza kuilinda safu ya ulinzi na hilo ni jukumu kubwa kwa timu ambayo inataka kushambulia.” Alisema Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England.

Naye mlinzi wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amekoshwa na kiwango cha staa huyo kwa jinsi ambavyo anaulinda ukuta wa ulinzi wa Arsenal kama ambavyo viungo wa enzi zao walikuwa wanafanya kwa ajili ya kuisaidia kazi safu ya ulinzi.

“Zamani tulizoea kuwatumia viungo wetu kama ngao. Hicho ndicho ambacho Torreira anafanya. Anaweza kuwa gundi ya timu hii ya Arsenal” alisema Keown ambaye alimfananisha staa huyo na viungo wao wa zamani wa ulinzi akina Patrick Vieira na Gilberto Silva.

Kwa sasa Arsenal inashika nafasi ya tano kufuatia ushindi wa mabao 3-2 wa Tottenham dhidi ya Wolves lililochezwa mara baada ya kumalizika kwa pambano lao dhidi ya Liverpool Jumamosi usiku. Hata hivyo kiungo mwingine wa Arsenal, Granit Xhaka amedai kwamba wachezaji wengi wa timu hiyo wana uhakika kuwa Arsenal itamaliza katika nafasi nne za juu.

"Kila mechi tunajua ambacho tunatakiwa kufanya. Tunawajua maadui vizuri, tunajua uzuri wao na ubovu wao. Emery ni muhimu sana. anatusaidia sana, sio mimi tu lakini pia na wachezaji wengine. Anatusaidia kila kitu. Anatusaidia mbinu. Unaweza kuona hilo katika mechi. Mambo mengi yamebadilika. Sasa hivi tunapambana. Kama umefungwa 1-0 kwa mfano na timu kama Liverpool, tunarudisha na hilo sio mara ya kwanza.” Alisema Xhaka.

“Tulijua tusingepoteza pambano dhidi ya Liverpool kwa sababu tulikuwa wazuri sana na tulionyesha upambanaji tena. Ukiitazama mechi hii vizuri utajua kwamba tupo tayari kwa ajili ya kwenda Top Four.” Alisema staa huyo wa kimataifa wa Uswisi.

Ferdinand afichua siri ya Arsenal, ni Torreira

LONDON, ENGLAND

ARSENAL wanachekelea wanachokiona kwa sasa katika timu yao. Lakini Rio Ferdinand, mlinzi wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England amedai kwamba anajua sababu ya msingi ambayo inawafanya Arsenal wachekelee.

Advertisement