Fei Toto aanza hesabu upyaaa

Muktasari:

  • Fei alikiri Azam wapo vizuri kwani ina nyota wenye uwezo wa hali ya juu, aliwatumia salamu kwamba watakumbana na muziki mnene kutoka kwao.

KAZI inaanza upyaa kwa kiungo nyota wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amesema wanaenda kucheza dhidi ya Azam FC, akiwa na tahadhari ya kuepuka kadi zitakazokuwa ndani ya uwezo wake, lengo ni kuhakikisha timu yake inapata pointi tatu muhimu.

Fei Toto ni kati ya wachezaji wa Ligi Kuu Bara ambao wamelimwa kadi nyingi za njano msimu huu na yeye amelifafanua kuwa wakati mwingine hata hajui anapewaje wakati anakuwa akiwania mpira.

“Kuna kadi nyingi ninazopata huwa nawashangaa waamuzi kwani sijui ninakosea wapi, lakini nyingine zinakuwa za haki zinazotokana na aina ya mchezo unavyokuwa,” alisema na kuongeza;

“Tunaenda kucheza na Azam, najua itakuwa mechi ngumu itakayohitaji ushindani wa hali ya juu na umakini ambao ndio utakaoamua mechi, kikubwa Yanga tunahitaji pointi tatu ili kuendelea kujiweka mazingira ya ubingwa, kikubwa kwangu kazi ndiyo inaanza upya,” alisema.

Fei alikiri Azam wapo vizuri kwani ina nyota wenye uwezo wa hali ya juu, aliwatumia salamu kwamba watakumbana na muziki mnene kutoka kwao.