Fei Toto: Marefa wananionea kunipa kadi za njano

Wednesday June 26 2019

 

By Khatimu Naheka

Cairo, Misri. Kiungo wa Taifa Stars, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema kupata kwake kadi mara kwa mara ni mapungufu ya waamuzi.

Feisal amesema amegundua hilo mapema juu ya marefa na kwamba ameanza kujipanga kukwepa kadi hizo.

Feisal amesema waamuzi wengi wamekuwa wakimharibia kwa kumpa kadi za mapema ingawa sio mchezaji anayecheza vibaya.

Amesema tayari ameshakutana na kocha Emmanuel Amunike ambaye amemsisitiza juu ya kupunguza kupata kadi mara kwa mara.

Amesema anachopenda ni kucheza kwa jihadi, lakini hana dhamira ya kucheza vibaya akiwa uwanjani.

Akizungumzia kutolewa katika kipindi cha kwanza huku akishambuliwa katika mitandao Feisal amesema hilo halimpi shida kutokana na baada ya matokeo mazuri kelele zitaisha.

Advertisement

Advertisement