Fedha za MO zawatesa AS Vita

Muktasari:

Manara amesema mpira wa Afrika unatawaliwa na fitna nyingi ambazo Simba imejipanga kupambana nazo.

Simba imeonyesha jeuri kubwa baada ya kutumia hoteli mbili kubwa ndani ya siku mbili.
Simba mara baada ya kufika jana ilitua katika ya Venus na kulala hapo kwa siku moja.
Baada ya kufika mchana Simba wakakubaliana kuhama hoteli hiyo na kutua hoteli nyingine kubwa ya Royal.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema akili hiyo ya kuhama hoteli ni kuhakikisha hawafanyiwi hujuma na kuwapa shida wapinzani wao.
Manara amesema mpira wa Afrika unatawaliwa na fitna nyingi ambazo Simba imejipanga kupambana nazo.