Faini ya CAF Simba na Yanga haikwepeki

Muktasari:

Faini hiyo ni baada ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Cliford Ndimbo kutolea ufafanuzi kuwa dirisha la usajili kwa mashindano hayo makubwa ya CAF limefungwa tangu Julai 10.

SUALA la faini kwa washiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika ipo pale pale.
Hii ni kwa klabu nne ambazo zinawakilisha Tanzania katika michuano hiyo, Simba na Yanga ambazo zitashiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na KMC  wao wanashiriki Kombe la Shirikisho.
Faini hiyo ni baada ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Cliford Ndimbo kutolea ufafanuzi kuwa dirisha la usajili kwa mashindano hayo makubwa ya CAF limefungwa tangu Julai 10.
"Baada ya tarehe hiyo hadi Julai 21 timu itakayochelewa italipa dola 250 (zaidi ya Sh 500,000), Itakayochelewa hadi Julai 31 itatoa faini ya dola 500 (zaidi ya Sh 1 milioni)," alisema Ndimbo.
Amesema, kwa klabu itakayosajili baada ya Julai 21, wachezaji wao wataanza kucheza mzunguko wa pili wa mashindano hayo.