ligi kuu daraja kwanza, Kassana Jonathan

RATIBA ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) imetangazwa leo Ijumaa Septemba 22 ambapo itaanza Oktoba 9 mwaka huu itachezwa katika makundi mawili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya ligi ya Bodi ya Ligi nchini (TPLB), Kassana Jonathan amesema ligi hiyo itashirikisha timu 20.

Amesema timu hizo zitagawanywa katika makundi mawili ambapo kila kundi litakuwa na timu 10.

Kundi A, litakua na timu za Africa Lyon, African Sports, Boma Fc, Gipco Fc, Lipuli Fc, Mawenzi Market, Majimaji Fc, Ndanda, Mbeya Kwanza na Njombe Mji.

Kundi B kutakuwa na timu ya Alliance, Arusha Fc, Fountane Gate, Geita Gold,  Kitayose, Mbao Fc, Pamba Fc, Rhino Rangers, Singida United, na Trans Camp.

Mechi za kwanza zitachezwa Oktoba 9, 10 na 11 mwaka huu kwa makundi yote ambapo mchezo wa kwanza kundi A, utazikutanisha African Lyon na Ndanda huku kundi B, watacheza Fountane Gate dhidi ya Alliance.

Katika mkutano huo, Mhamasishaji wa ligi hiyo Pascal Kapombe amewataka mashabiki kutoa sapoti kwa timu zote pale itakapohitajika.

“Tuonyeshe sapoti kwa timu zote ili tupate burudani safi na yenye viwango vya  juu kama ilivyo Ligi Kuu Bara," amesema Kabom