Eymael atamani Uwanja wa Taifa

Friday January 17 2020

Eymael atamani taifa yashindikana-KOCHA mpya wa Yanga- Luc Eymael -uwanja wa Taifa-Ligi Kuu Bara-

 

By Thobias Sebastian

KOCHA mpya wa Yanga, Luc Eymael amesema alitamani kikosi chake kingefanya mazoezi leo Ijumaa kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Taifa, lakini imeshindikana.
Amesema kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake hilo limeshindikana
Eymael alilimbia Mwanaspoti leo Ijumaa kuwa aliwapa taarifa viongozi wake alitamani timu afanye mazoezi Uwanja wa Taifa ambao, utatumika katika mechi ya kesho Jumamosi usiku ambayo watacheza dhidi ya Azam FC katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara.
"Hata ukiangalia kanuni za soka tulitakiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa mechi, lakini kwa kuwa nimepewa sababu za kushindikana kufanya mazoezi hapo," alisema.
"Tutafanya mazoezi mapesi na kuwapatia maelekezo wachezaji wangu ili kufanya vizuri dhidi ya Azam FC ambao, nimewafatilia na kubaini wana kikosi kizuri jambo ambalo litatupa ushindani," alisema Eymael.
Azam ambao kwa sasa wanatumia Uwanja wa Taifa baada ya ule wa Azam Complex kuwa katika matengenezo, watakutana na Yanga iliyotoka kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Advertisement