Everton yamvuta beki Man United

Muktasari:

Man United ilipanga kumpa nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja, lakini hajatia saini baada ya kudai maboresho ya mshahara akitaka Pauni 90,000 kwa wiki. Endapo pande hizo zitashindwa kufikia mwafaka, Everton inaweza kumsajili Smalling katika dirisha dogo.

London, England. Everton imetuma maombi ya kumsajili beki wa kati wa Manchester United, Chris Smalling.

Klabu hiyo inataka kumsajili Smalling akiwa mchezaji huru, baada ya mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi msimu ujao.

Man United inaweza kumpiga bei Smalling mwenye miaka 28, baada ya kushindwa kucheza kwa kiwango bora msimu huu.

Jose Mourinho ameanza mchakato wa kusaka beki mpya wa kati katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

Harry Maguire wa Leicester City, anawindwa kwa nguvu na Mouringo katika usajili wa dirisha dogo, baada ya kucheza kwa kiwango bora kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Smalling anatambua nafasi yake Man United ni ndogo, hivyo anaweza kufanya uamuzi mgumu wa kuondoka Old Trafford majira ya kiangazi.

Man United ilipanga kumpa nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja, lakini hajatia saini baada ya kudai maboresho ya mshahara akitaka Pauni 90,000 kwa wiki.

Endapo pande hizo zitashindwa kufikia mwafaka, Everton inaweza kumsajili Smalling katika dirisha dogo.

Chanzo ndani ya klabu hiyo kilidai beki huyo anawindwa na klabu mbalimbali Ulaya, lakini Everton inayotoka Goodison Park imeonyesha dhamira kubwa.

“Chriss atakuwa nje ya mkataba msimu ujao, anaendelea na mazungumzo, lakini hadi sasa hawajafikia mwafaka,” kilisema chanzo hicho.