Eto’o ashusha neema uwanja Kinondoni

Muktasari:

Eto’o amekuja nchini kama Balozi kwa udhamini wa Castle Lager ikiwa chini ya Tanzania Breweries Limited kwa lengo la kuendeleza soka nchini.

Dar es Salaam. Ujio wa mshambuliaji Samuel Eto’o umeshusha neema kwa Manispaa ya Kinondoni baada ya Manispaa hiyo kuhakikishiwa kupata uwanja kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya soka nchini.

Kupitia kwa Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta alisema wanashukuru kupata udhamini huo kwa kujengewa uwanja ndani ya Manispaa yao.

"Hili jambo ni zuri na tunafuraha kwamba limekuja kufanyika katika Manispaa yetu, jambo kubwa zaidi uwanja huu utatoa fursa kwa vijana kuendeleza soka lao," alisema.

Sitta aliongeza kwamba anatambua  vijana wengi wanapenda mpira hivyo watakuwa wakifika uwanjani hapo na kufanya mazoezi kisha wataenda katika fukwe ya Coco  kuweka miili yao sawa.

Ramani ya uwanja huo inaonyesha kutakuwa na viwanja vinne vya mazoezi.