Eti wa kwanza Messi wa pili Eden Hazard!

Tuesday September 11 2018

 

BEKI wa Chelsea, Antonio Rudiger amesema anavyoliona soka la sasa lilivyo, supastaa wa timu yao Eden Hazard kama kuna mchezaji anampiku kwa ubora basi ni Lionel Messi peke yake.

Mjerumani huyo alisema hapa duniani kwa sasa kuna mchezaji mmoja tu anayemzidi kiwango Hazard na ni staa wa Barcelona na Argentina, Messi.

Rudiger ameamua kuwaondoa kwenye orodha kabisa mastaa wengine matata kama Cristiano Ronaldo, Neymar na Kylian Mbappe na kusema Hazard ni kiboko ya wote hao.

“Mbappe ana kasi sana, ni mzuri pia. Kumzuia, mnapaswa kulifanya jukumu hulo kama timu kwa sababu peke yako utasumbuka. Lakini, kwa upande wangu, ukiambia mchezaji bora kwa sasa ni nani nitakwambia Messi, kisha anayefuatia ni Hazard.”

Rudiger alichezeshwa beki wa kushoto kwenye mechi ya dhidi ya Ufaransa, eneo ambalo hajawahi kucheza sana, lakini alionyesha kiwango bora na kusema yeye anacheza popote pale ambako kocha atampanga na kumtaka acheze.

Advertisement