Eti Unai Emery kaimaliza Arsenal

Muktasari:

  • Arsenal jana Jumapili ilitarajia kumenyana na Manchester United kwenye Ligi Kuu England huko Emirates, lakini mechi hiyo imekuja siku chake tangu ilipotoka kuchapwa 3-1 na Rennes kwenye Europa League, Alhamisi iliyopita.

LONDON, ENGLAND.STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Charlie Nicholas amedai timu hiyo imepiga hatua kibao nyuma tangu Kocha Unai Emery alipotua kuchukua mikoba ya Arsene Wenger huko Emirates.

Staa huyo alisema haoni kitu chochote kilichokuwa tofauti na zaidi tu timu kuwa nyepesi na inafungwa hovyo kabisa tofauti kabisa na ilivyokuwa kipindi cha Mfaransa Wenger kwenye kikosi hicho.

Arsenal jana Jumapili ilitarajia kumenyana na Manchester United kwenye Ligi Kuu England huko Emirates, lakini mechi hiyo imekuja siku chake tangu ilipotoka kuchapwa 3-1 na Rennes kwenye Europa League, Alhamisi iliyopita.

Kipigo hicho kinakiacha kikosi hicho cha Emery sasa kupambana kuhakikisha kinafanya kweli kwenye mechi ya marudiano.

“Nimekuwa nikisema hili muda wote,” alisema Nicholas. “Kwenye beki wapo hovyo, hovyo kwelikweli, hawana kiongozi na wanachezacheza tu.”

“Hata (Petr) Cech kashuka kiwango. Nilichokiona kinatosha, kwa sababu tangu alipokuja Arsenal, hakuna kilichofanyika, mambo ndio kwanza yamekuwa magumu.”