Eti! Yanga ya Zahera kiwango kimeshuka saana

Muktasari:

Yanga ambayo iliongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kipindi kirefu lakini Simba ambao ni mabingwa watetezi waliwashuka hadi nafasi ya pili. Kwa sasa Yanga ni ya pili na ina pointi 80 na Simba inaongoza na  pointi 81.

Dar es Salaam. Kocha wa Biashara United, Amri Said ametoa maneno mazito ambayo bila shaka hayawezi kumfurahisha Kocha wa Yanga Mkongo Mwinyi Zahera.
Amri mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars kabla ya kujikita kwenye ukocha.
Amesema, ameshangaa kuona kiwango cha kikosi cha Yanga kimekuwa kikishuka kila siku.
"Yanga ya sasa si ile ya zamani tunayoijua, lakini sasa hivi ni tofauti. Na hata mimi ilikuwa rahisi kuwafunga kwa sababu aina ya mpira wao niliuona walipocheza na Lipuli Iringa,"alisema Amri kocha wa zamani wa Lipuli FC aliondoka na kujiunga na Mbao FC kabla ya kutua Biashara.
"Wanacheza mipira mirefu na ndivyo walivyocheza hata walipokuja kwetu ikawa rahisi kuwazuia."
Amesema, Yanga ya zamani ilikuwa na kasi na walikuwa wanacheza mpira wa pasi fupi na ndefu. 
Maneno hayo ya Amri ni baada ya mchezo wao na Yanga kumalizika ambapo Biashara United waliibuka na ushindi wa bao 1-0, mechi ikichezwa Uwanja wa Karume mkoani Mara.