Eti! Red Stars walibet kufungwa na PSG

Muktasari:

  • Ushindi wa PSG dhidi ya Red Stars yalikuwa matokeo makubwa zaidi katika michezo ya Ligi ya Mabingwa katika usiku wa Oktoba 3-4.

Paris, Ufaransa. Polisi nchini Ufaransa imeanza kufanya uchunguzi madai ya kuwepo kwa upangaji matokeo katika ushindi wa Paris St-Germain wa mabao 6-1 dhidi ya Red Star Belgrade katika Ligi ya Mabingwa mwezi uliopita.
Taarifa zinadai kuwa kuna kiongozi wa Red Star ameshinda mchezo wa kubahatisha ‘bet’ zaidi ya pauni4.3milioni kwa kubashiri kuwa klabu hiyo ya Serbia itafunga mabao matano liliripoti gazeti la L'Equipe.
Mamlaka ya Taifa ya uchunguzi nchini Ufaransa (PNF) wameanza kufanya uchunguzi baada ya kupokea madai kutoka Uefa.
Klabu zote mbili zimekataa kuhusika na suala hilo.
PSG ipo nafasi ya tatu katika Kundi C, ikiwa nyuma ya Liverpool, lakini wakilingana kwa pointi tatu baada ya mechi mbili. Red Star (ina pointi moja) ikiwa mkiani wakati Napoli inaongoza.
Red Star imetoa taarifa: "FC Red Star imeshangazwa na taarifa hiyo na inapiga vikali madai hayo.
"Taarifa imeharibu sifa na heshima ya klabu hiyo na ndiyo sababu tunasisitiza Uefa ije ifanye uchunguzi na hapa Serbia pamoja na Ufaransa ili kupata ukweli wa suala hii.
Katika mchezo huo Oktoba 3, mshambuliaji Neymar alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ na Edinson Cavani, Angel di Maria na Kylian Mbappe kila mmoja alifunga bao moja kwenye Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.
Huku Marko Marin akifnga bao la kufutia machozi kwa Red Star.