England yaweka rekodi

London, England. Uwepo wa Reece James katika timu ya taifa ya England uliingia dosari baada ya beki huyo kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Denmark juzi usiku.

Beki huyo wa kulia wa Chelsea alikuwa na mchezo mzuri katika kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley, lakini alijikuta akimaliza mchezo vibaya kwa kadi hiyo kutokana na kumtolea mwamuzi maneno.

Mambo yalikuwa mabaya baada ya filimbi ya mwisho, wakati beki huyo alipomfuata mwamuzi akimlalamikia kwa hasira.

James alionwekana akimsogolea mwamuzi hadi usoni kwa maneno ya ukali, kitu kilichomfanya mwamuzi kutosita na haraka alitoa kadi nyekundu mfukoni.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa wachezaji wawili kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo mmoja, wakati mwamuzi Jesus Gil Manzano alipomalizana na James baada ya filimbi ya mwisho.

Awali, beki wa kati na nahodha wa England, Harry Maguire alionyeshwa kadi mbili za njano zilizosababisha nyekundu kwa rafu alizocheza dakika ya 31.

Kocha Gareth Southgate aliiambia Sky Sports: “Mwamuzi alisema alimwonyesha (Reece James) kadi nyekundu kutokana na nidhamu, na bila shaka hilo ni somo kwake kwani bado kijana mdogo.”