England yaipiga mkono Kosovo, Sterling hakamatiki

Wednesday September 11 2019

 

By Eliya Solomon

Baada ya Valon Berisha kufungwa bao ndani ya sekunde 35, timu ya Taifa ya England iilibadilika na kuichakaza Kosovo kwa mabao matano katika dakika 45 za kipindi cha kwanza katika ushindi 5-3, huku Raheem Sterling na Jadon Sancho waking’ara kwenye mchezo huo.

Berisha aliwaduwaza England baada ya kuifungia Kosovo bao la kuongoza ndani ya sekunde 35, lakini goli hilo halikudumu baada ya Sterling kuisawazishia England katika dakika 8, Harry Kane alifunga bao la pili dakika ya 19. Sancho aliyeanza katika nafasi ya Marcus Rashford alimlazimisha, Mergim Vojvoda akajifunga.

Baadae Sancho anayechezea Borussia Dortmund ya Ujeruman alifunga bao la pili na kukamilisha mabao matano ya England ambayo Sterling alihusika kwa kiasi kikubwa kwa kutengeneza kwa pasi zake za mwisho.

Katika mchezo huo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Ulaya mwakani, Kosovo waliingia wakiwa na rekodi ya kutopoteza kwenye michezo yao 15 iliyopita.

Mabao mengine ya Kosovo kwenye mchezo huo yaliyofungwa kipindi cha pili, wafungaji wao ni Berisha (49) na Vedat Muriqi (55).

Changamoto kubwa ambayo imeonekana kwenye kikosi cha Gareth Southgate ni kwenye safu yao ya ulinzi ambayo ilishindwa kuendana na kasi ya mashambuilizi ya Kosovo kiasi cha kuruhusu mabao matatu kwenye mchezo huo.

Advertisement

Baada ya mchezo huo, Southgate alionyeshwa kutovuitiwa na kiwango cha timu yake kwa kudai walikuwa na makosa mengi kwa mchezaji mmoja mmoja ambayo yangewagharimu.

“Tumefanya makosa mengi kitu muhimu ni kuondokana na makosa hayo, Raheem Sterling amekuwa kwenye kiwango bora. Sio rahisi kumzuia,” alisema kocha huyo.

Naye Sterling aliyefunga bao moja na kutengeneza matatu, alisema kiwango ambacho alikionyesha kwenye mchezo dhidi ya Kosovo akiwa na England ni kiwango chake bora zaidi.

 

Advertisement