Emery akiri ngoma ngumu Arsenal

Muktasari:

  • Kitu kingine kinachomtisha Emery ni kasi ya Man United, ambapo kwa sasa imeshinda mechi zake zote tangu ilipoanza kuwa chini ya Kocha Ole Gunnar Solskjaer huku ikiwa bado ina mechi ya kubaliana wenyewe kwa wenyewe.

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal, Unai Emery amekiri kwa sasa ngoma ni ngumu kwa timu hiyo kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kupigwa na West Ham United.

Kikosi hicho cha Emery kilikumbana na kipigo kutoka kwa West Ham, shukrani kwa bao la Declan Rice ambalo limewafanya Hammers kushinda, lakini likipeleka majanga ma Emirates, ambapo sasa wanalingana pointi na Manchester United kwenye msimamo wakichuana kufukuzia Top Four.

Chelsea wanaoshika nafasi ya nne, kwa sasa wapo juu kwa pointi sita, kitu ambacho Emery anaona ni kigumu katika kukamatia wapinzani wao hao nan kutinga Top Four kutokana na mwendo wa kikosi chake ulivyo.

Kitu kingine kinachomtisha Emery ni kasi ya Man United, ambapo kwa sasa imeshinda mechi zake zote tangu ilipoanza kuwa chini ya Kocha Ole Gunnar Solskjaer huku ikiwa bado ina mechi ya kubaliana wenyewe kwa wenyewe.

“Kwa sasa hali ni ngumu, hilo lipo wazi,” alisema Kocha Emery.

“Nafikiri kitu muhimu kwetu ni kurudi kwenye kiwango chetu na kuanza kushinda tena. Tunahitaji kuwa makini hadi mechi ya mwisho. Kama tutashinda, tukicheza na Chelsea mechi ijayo, hapo kutakuwa na pengo la pointi tatu. Kila kitu kipo kwenye uamuzi wetu wenyewe. Haya matokeo yetu ya sasa, yanaweka ugumu mkubwa.”