Ebwana! Wacameroon watangulia Kombe la Dunia

Muktasari:

Hayo ni mashindano ya vijana chini ya miaka 17 Afrika ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja viwili vya Chamazi na Taifa. T: Cameroon ipo Kundi B katika fainali za vijana za Afrika chini ya miaka 17.

 Dar es Salaam. Ukiwaona wachezaji wa Cameroon kimwonekano katika mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ya AFCON ni unaweza kusema ni vijeba kwa sababu maumbo yao ni makubwa sana sasa kocha wao mkuu, Thomas Libiih amefunguka kila kitu.

Libiih amesema, watu wasiwe na wasiwasi na wachezaji wake kwa sababu wana umri sahihi wa mashindano na ukubwa wa maumbile yao una sababu. Ametaja sababu hiyo ni kwamba, wachezaji wake wanakula sana chakula na huwa hawatanii kabisa kila wanapokuwa katika maeneo hayo.

"Kile ni chakula tu hakuna kitu kingine. Watu wasiwe na wasiwasi kabisa, wakitaka wachezaji wao wawe kama wa kwangu wawazingatie mambo ya msosi,"alisema Libiih. Amesema, aina ya chakula ambacho wanakula ni fufu (ugali wa mhogo , aliko (ugali wa mahindi), mihogo yenue kwa wingi na garry (aina ya chakula cha mhogo pia).

Amesema, pamoja na miili hiyo mikubwa, wachezaji wake hawafanyi mazoezi ya gym kwa sababu bado wadogo. "Wale ni wachezaji wadogo kiumri, ukiwafanyisha mazoezi ya gym unawaharibu. Gym si mazoezi sahihi kwa vijana wadogo na haitakiwi katika makuzi ya vijana,"aliongeza Libiih.

Hayo ni mashindano ya vijana chini ya miaka 17 Afrika ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja viwili vya Chamazi na Taifa. T: Cameroon ipo Kundi B katika fainali za vijana za Afrika chini ya miaka 17.

Tayari imefuzu nusu fainali baada ya kuifunga Guinea na Morocco, imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Senegal ambayo pia imeshafuzu.